Harnaam Kaur mwenye miaka 23 ni mwalimu msaidizi wa zamani toka U.K. Na kilichotokea tu ni kwamba anajivunia hali kuwa na ndevu kama mwananume.
Harnaam Kaur ana hali ambayo kitaalamu inaitwa polycystic ovary syndrome inayomfanya ukuwaji wake wa nyweli kwenye mwili wake ufananane na wa mwanaume na alikuwa na miaka 11 ndipo hali hiyo ilipoanza kumtokea.
Alijaribu kuwa anazikata hata mara mbili kwa wiki na kutumia namna mbalimbali kuweza kuizuia hali hiyo ila hakuna alichofanikiwa.
Shuleni wenzake walikuwa wakimshangaa huku wakimuita majina mbalimbali ya utani kama "beardo" na "she-male". Hata ilifikia hatua ambapo alikuwa anaogopa kutoka chumbani kwake kutokana na mawazo aliyokuwa akiyapata kwa vile watu wanavyomchukulia.
Ila baadaae, akiwa na miaka 16, Harnaam alibatizwa na kuwa mfuasi wa Sikh na kutokana na imani za dini hiyo ilibidi aache kuwa anazinyoa ndevu zake kama ambavyo dini hiyo inavyotaka kwa imani yake.
Cheki picha zake nyingine hapo chini...
No comments:
Post a Comment