Saturday, May 25, 2013

Wanawake Wenye Tattoo Ni Rahisi Zaidi Kufanya Mapenzi Kwenye Siku Ya Kwanza (UCHUNGUZI)

Najua wanawake wengi wanaweza kutoipenda hii habari (Hasa wale wenye tattoo). Ila kwa mujibu wa Profesa mmoja wa Kifransa amesema, kama wewe ni msichana mwenye tattoo ni rahisi ukalala na mwanaume siku ya kwanza mnapokutana.
 
Pia amesema wanawake wenye tattoo huwa ni wenye mvuto zaidi ni rahisi kuingilika.
 
Matokeo ya utafiti huo yamekuja baada ya timu kutoka Chuo cha de Bretagne-Sud cha nchini Ufaransa kuzunguka na kupita kwenye fukwe mbalimbali na kuja na matokeo hayo.

Wanawake 11 wenye umri kiasi wamegundulika kuwa ndio wenye mvuto zaidi nje ya kundi la wanawake 58 waliotembelea fukwe mara 20 katika kipindi cha majira ya joto, na asilimia 50 kati yao huweka tattoo za muda chini kidogo nyuma ya miili yao, tattoo ambazo baadae huwa wanakuja kuzifuta.

No comments:

Post a Comment