Tuesday, April 08, 2014

INASTAAJABISHA: Simba Amuuwa Nyani Jike, Ila Alichokifanya kwa Mtoto Wake Inashtusha [PICHA]

Wapiga picha wawili Evan Schiller na Lisa Holzwarth walikuwa kwenye shughuli zao za kitalii Kaskazini mwa nchi ya Botswana na kwa mbali wakaliona kundi kubwa la nyani kama thelathini au arobaini hivi wakiwa kwenye pilika pilika.

Ikaja kuonekana kwamba nyani hao kumbe walikuwa wakichokozana na simba wachache waliokuwa wanawawinda. Simba walikuwa wakiunguruma huku nyani wakiwa wanapiga kelele, kwa wastani ulikuwa ni mvurugano.

Cha kushangaza sasa, wapiga picha hao wawili walifanikiwa kuchukua picha za tukio moja la kushangaza sana wakati vurumai hiyo ikiwa inaendelea.

Cheki hapo chini  picha kamili...


Nyani wa kike alijaribu kukimbia ila kwa bahati haikuwa yake siku hii. Kwa maana simba huyu aliwahi kumkamata na kumuweka kwenye himaya yake.



Ghafla, nyani yule mtoto akawa anataka kukimbia ila hakuwa na nguvu za kupanda mti. Simba akaamua kwenda kuangalia nini hasa kilikuwa kinaendelea.



Hakika alikuwa na roho na mstaarabu, kwa maana cha kushangaza badala ya kwenda kumuua, simba huyu alianza kucheza na nyani mtoto.



"Cha kushangaza zaidi ni vile ambavyo nyani huyu mtoto alivyokuwa akimkumbatia simba kifuani kwake  hata kufikia hatua kama ya kutaka kunyonya. Mtoto alikuwa akionyesha dalili za mguso wa mzazi. Huku simba akimuweka karibu na mdomo wake kama vile anavyokuwa akimlea mtoto wake."


Ghafla, wakatokea simba wawili kwenye eneo la tukio. Ila simba huyu mlezi alionekana kutojali juu yao. Je alikuwa akijaribu kumlinda mtoto mpya aliyempata?



Kwa muda wote, baba wa nyani yule alikuwa akiangalia tukio zima toka kwa mbali huku akisubiri muda muafaka ili amuokoe mtoto wake. Na hatimaye alifanikiwa kwenda kumkomboa mwanaye.


Umeguswa na kujifunza vipi juu ya tukio hili...?

No comments:

Post a Comment