Sunday, June 15, 2014

Ungependa Kuwa Muwakilishi wa Tanzania Kwenye Shindano la Big Brother Mwaka Huu...? Hii Inakuhusu

Kampuni ya MultiChoice Africa inayoandaa mashindano ya Big Brother Africa imetangaza tarehe ya usaili wa shindano hilo mwaka huu katika nchi mbalimbali za Afrika.

Waandaaji hao wameitaja nchi ya Rwanda mwaka huu kuwa miongoni mwa nchi zitakazokuwa na washiriki katika shindano hilo mwaka huu ambapo mshindi ataondoka na kibunda cha $300,00.

Tuesday, June 10, 2014

Jennifer Lopez Kutoimba Kwenye Ufunguzi wa Kombe la Dunia

Mwanamuziki Jennifer Lopez hatoweza kuimba wimbo rasmi wa Kombe la Dunia kwenye sherehe za ufunguzi wa michuano hiyo nchini Brazil, Fifa imetangaza.

Monday, June 09, 2014

Filippo Inzaghi Achukua Nafasi ya Clarence Seedorf Kuifundisha AC Milan

Klabu ya AC Milan amemfukuza kazi kocha wake Clarence Seedorf baada ya kipindi kisichozidi miezi mitano toka ashike nafasi hiyo, huku ikimtaja Filippo Inzaghi kama mrithi wake.

Mchezaji huyo wa zamani wa Italia Inzaghi, 40, amesaini mkataba wa miaka miwili kuifundisha timu hiyo huku akiachana na kazi ya kufundisha timu ya vijana ya timu hiyo.

Happy Birthday: The Kokomaster D'Banj Atimiza Miaka 34 Leo

Mkali toka Naija, Dbanj leo ameongeza mwaka mwengine kwenye maisha yake. Hongera kwake na wote waliozaliwa siku na tarehe kama hii akiwemo Chris Wamarya...!

Kim Kardashian Asema Kanye West Ameyabadili Maisha Yake [Ujumbe wa Birthday]

Mnamo siku ya Jumapili Kanye alitimiza miaka 37, mke wake Kim Kardashian alitumia mtandao wa kijamii kusherehekea naye huku akiweka wazi kwa kuandika ujumbe kwamba "Kanye ameyabadilisha maisha yake kwa njia nyingi. Haishangazi kuona havai kihivyo." lol!

Sunday, June 08, 2014

Msichana wa Bongo Movie Aliyedaiwa Kula Uroda na Mbunge Akana Kuwa Sio Yeye Kwenye Picha HizoPicha chafu zinazodaiwa kuwa za star wa filamu nchini Shamsa Ford na mbunge wa Chadema, Salvatory Machemli, zimeanza kusambaa kwa kasi mitandaoni tangu jana.

Picha hizo zinawaonyesha wawili hao wakiwa kitandani kwenye mahaba mazito, hata hivyo picha hizo zinaonekana kutia shaka kuwa sio halisi ni za kutengenezwa ingawa hatuna uhakika kwa asilimia zote kwasababu msichana anayedaiwa kuwa Shamsa Ford ana umbo tofauti na la star huyo.

Diamond Ashindwa Kupata Tuzo za MTV Base

Msanii aliyekuwa akiiwakilisha Bongo kwenye tuzo za MTV Base, Diamond Platnumz ameshindwa kutwaa tuzo mara baada ya tuzo alizokuwa akigombania kuchukuliwa na wanamuziki toka nchi nyingine.
Tuzo ya Best Collaboration ilichukuliwa na Uhuru na wimbo wake uitwao Tjukutcha ambayo amemshirikisha Professor Oskido & Dj Bucks huku tuzo Best Male ikienda kwa Davido kutoka nchini Nigeria.

Kauli ya Kwanza ya Diamond Mara Baada ya Tuzo za MTV Base

Mara baada ya kumalizika kwa tuzo za Mtv Base huku mwanamuziki aliyewakilisha Bongo Diamond Platnumz kushindwa kupata tuzo, kupitia ukurasa wake wa Facebook msanii huyo aliandika hili kama kauli yake ya kwanza.

Mzee Small Afariki Dunia

Muigizaji mkongwe nchini Said Ngamba maarufu kama Mzee Small amefariki dunia siku ya Jumamosi majira ya saa 4 usiku akiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar.

Thursday, June 05, 2014

Kutaka Kuwa na Makalio Makubwa Kumemponza Dada Huyu, Hebu Mcheki Alivyoharibika

Kwa wale wadada wanaotumia dawa za uongeza makalio yao wakiamini kuwa ndio wataonekana wazuri na kuwavutia wanaume, au haujatumia ila unafikiria kutumia siku moja,angalia hapa alafu utapata jibu utumie au ubaki na maumbile yako ya halisi

Chanzo: Hotnewzdaily

Ndoa ya Flora Mbasha Yalala Chali, Flora Adaiwa Kuhamia kwa Gwajima

Flora Mbasha akiwa na mumewe Emmanuel Mbasha.
BAADA ya kudumu kwa zaidi ya miaka 10, imebainika kuwa ndoa ya mwanamuziki mahiri wa muziki wa Injili Bongo, Flora na mumewe Emmanuel Mbasha ipo chali kwa maana ya kuanguka huku ikidaiwa kuwa, kusimama imara tena inawezekana lakini ni kazi kubwa, Amani limefukunyua mazito.
Hilo limejitokeza wiki moja baada ya madai ya mwanaume huyo kudaiwa kumbaka shemeji yake na kesi ipo polisi.

Wednesday, June 04, 2014

Je ni Kweli Kwamba Beyonce Ana Mahusiano ya Siri na Mlinzi Wake [PICHA]

Kwa mujibu wa taarifa za hivi karibuni, inasemekana kwamba Jay Z anapatwa sana na wivu kutokana na ukaribu wa Beyonce na mlinzi wake aitwaye Julius (mtalaka mwenye mtoto mmoja), akidhani kuwa wawili hao wana mahusiano.

Huyu ndiye yule yule mlinzi aliyejaribu kumlinda Jay Z dhidi ya shambilizi la kwenye lifti. Jamaa yupo karibu sana na Beyonce, mara zote mikono yake huwa ipo karibu ya mwanamuziki huyo.

Tuesday, June 03, 2014

Joseph Olita Aliyeigiza Kama Idi Amin Amefariki

Muhusika mkuu aliyevaa tabia za dictator Idi Amini kwenye filamu ya Rise and Fall of Idi Amin, Joseph Olita amefariki dunia mnamo siku ya Jumapili, June 1, akiwa na umri wa miaka 70.

Imeripotiwa kuwa Olita alikuwa anasumbuliwa na shinikizo la damu na alizidiwa siku hiyo hiyo ya Jumapili akiwa nyumbani kwake wilaya ya Siaya nchini Kenya na kupoteza maisha majira ya saa tano asubuhi.

Angalia Alichokivaa Rihanna Kwenye Shughuli Hii [PICHA]

Cheki picha zaidi hapo chini..

David Beckham Anafikiria Kurudi na Kuendelea Kucheza Soka

David Beckham amesema anafikiria kurudi na kuendelea kucheza soka. "Naanza kujifikiria binafsi je naweza kucheza tena? Hivi kweli naweza kurudi? Je nitaweza kutoka kwenye kustaafu na kuanza kucheza?'" alisema Beckham.

Monday, June 02, 2014

Etoo Ampa Kijembe Kingine Mourinho kwa Aina ya Mtindo ya Ushangiliaji wa Kibabu Kizee [PICHA]

Mchezaji huyo mwenye miaka 33 kwa mara nyingine tena ameonekana kumpa kijembe meneja wa timu ya Chelsea, Jose Mourinho, mara baada ya kufunga goli na kushangilia kwa mtindo wa kibabu kizee walipocheza dhidi ya Ujerumani siku ya Jumapili.

Thursday, May 29, 2014

Sugu Amvaa Zitto Kabwe Bungeni

Ni katika Hotuba yake ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ya Wizara ya Habari,Utamaduni na Michezo aliyoiwasilisha Bungeni leo hii muda mfupi uliopita. Waziri Kivuli Joseph Osmundi Mbilinyi aka Sugu amemtaja Zitto Z. Kabwe kama Mmiliki wa Kampuni ya Leka Dutigite aliyofanya biashara isivyo halali na Mashirika ya Umma ya NSSF na TANAPA. 

Sehemu husika ya Hotuba hiyo ni hii:

Malcolm Glazer Aliyekuwa Mmiliki wa Manchester United Afariki Dunia

Aliyewahi kuwa mmiliki wa klabu ya Manchester United, Malcolm Glazer, amefariki dunia mnamo siku ya Jumatano akiwa na umri wa miaka 85.

Glazer, aliyeinunua  United mwaka 2005, pia anamiliki timu ya kwenye ligi ya NFL iiitwayo Tampa Bay Buccaneers, ambao ndio waliotangaza habari ya kifo chake kwenye mtandao wao.

Wednesday, May 28, 2014

Mume wa Mwimbaji Nguli wa Injili Adaiwa Kumbaka Shemeji Yake


KWA UFUPI

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu
ya Dar es Salaam,Suleiman Kova
alisemahakuwa amepokea taarifa
yoyote ya aina hiyo.


Mume wa mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili, (jina tunalihifadhi kwa sasa), anatuhumiwa kumbaka shemeji yake mdogo (17).

Taarifa za tukio hilo ziliripotiwa juzi saa 12 jioni katika Kituo cha Polisi Tabata (Tabata Shule), zikimtuhumu mwanamume huyo kwamba alimbaka binti huyo mara tatu na kumsababishia maumivu makali.

Tuesday, May 27, 2014

Picha za Kwanza za Harusi ya Kim Kardashian na Kanye West Kama Wanandoa [PICHA]

Na sasa, ningependa kukuonyesha picha rasmi za harusi ya Kim Kardashian na Kanye West kama wanandoa rasmi.

Cheki picha zaidi hapo chini...

Sunday, May 25, 2014

Cheki Picha za Harusi ya Kanye West & Kim Kardashian [PICHA]

Hii ni mara ya tatu kwa Kim kuolewa ila kwa Kanye West hii ni mara ya kwanza. Hatimaye wawili hao walifunga pingu za maisha mnamo siku ya Jumamosi May 24 pande za Fort di Belvedere ndani ya Florence, Italy.

Baadhi ya wana familia na marafiki walikuwepo ila ni wale ambao Kanye West kweli aliwahitaji, na baadhi yao hawakufika. Jay Z na Beyonce wa waliingia mitini.

Cheki picha zaidi hapo chini...