Tuesday, April 08, 2014

Mcheki Daniel Sturridge Akiwafundisha Watoto Namna ya Kucheza Mtindo Wake wa Ushangiliaji [PICHA]

Hakika Sturridge amewashangaza walinzi wengi kwenye Ligi Kuu ya nchini Uingereza msimu huu kwa kasi na nguvu alizonazo, licha ya hivyo haikumfanya mshambuliaji huyu wa kushindwa kutenga muda wake japo kidogo kwa ajili ya kuwashangaza watoto wadogo wa shule moja iliyopo kwenye jiji la Liverpool.

Mshambuliaji huyo wa Uingereza alifika kwenye Shule ya Anfield Juniors Primary kwa ajli ya kufanya mahojiano ya kipindi cha Liverpool TV kiitwacho Kop Kids.

Sturridge aliwafundisha kila mtoto namna ya uchezaji wake wa kushangilia pale anapofunga goli kabla ya kuanza kujibu maswali yao.



No comments:

Post a Comment