Tuesday, April 08, 2014

Howard Web Apigwa Chini Kuchezesha Pambano la Liverpool na Man City Huku Mark Clattenburg Akipewa Nafasi

Refa toka Uingereza atakayechezesha Kombe la Dunia Howard Webb, amepata pigo baada ya kuondoshwa kuchezesha mechi kati ya Liverpool na Manchester City.

Webb, kwa kipindi sasa amekuwa akiteuliwa kuchezesha mechi za timu ya viwango vya chini toka alipopewa nafasi hiyo mara ya mwisho kwenye mechi ya FA kati ya Arsenal-Liverpool miezi miwili iliyopita kutokana na maamuzi yake mabovu, na wiki hii atakuwa ni muamuzi wa mechi kati ya Crystal Palace v Aston Villa badala ya kupewa nafasi ya kuchezesha mechi kali ya mwisho wa juma.


No comments:

Post a Comment