Wednesday, April 09, 2014

Baba wa Mtoto ni Nani? Yataarifiwa Rihanna ni Mjamzito [PICHA]

Kwa mujibu wa MediaTakeOut, jamaa wana taarifa kutoka kwa watu wa karibu sana na Rihanna na wamekuwa wakikusanya ushahidi ambao unaweza kuwa kweli.

Sababu ya kwanza waliyoitoa ni kwamba wiki chache zilizopita inaelezwa Riri ameacha kuvuta sigara na bangi, kitendo ambacho ni kinashangaza. Pia imeelezwa amekuwa akikataa mialiko ya party ambazo zina vilevi na bangi.

Kwa kuongeza, jamaa wameweka na picha inayomuonyesha akiwa nakunywa kile kinachohisiwa kuwa ni chai isiyokuwa na caffein akiwa na baba yake, Ronald Fenty, ndani ya L.A, kwenye mgahawa mashuhuri wa kahawa wa Starbucks.

Kuthibitisha zaidi, walitaka tumuangalie kwa karibu kwenye picha yake inayomuonyesha kama ni mjamzito hapo chini.

Kama kweli ni mjamzito, kuna uwezekano wa kuhusishwa mababa wawili hapa – Drake na Chris Brown.

No comments:

Post a Comment