Wednesday, April 09, 2014

Chelsea Yaiua PSG Dakika za Majeruhi na Kutinga Nusu Fainali [PICHA]

Goli la dakika za majeruhi lililofungwa na Demba Ba limeiwezesha timu ya Chelsea kuingia kwenye hatua ya nusu fainali ya michuano ya Klabu Bingwa Barani Ulaya mara baada ya kuifunga timu ya Paris St-Germain kwa wastani wa 3-3, huku timu ya Jose Mourinho ikifaidika na matokeo hayo kutokana na kuwa bao moja la ugenini walilolipata wiki moja iliyopita kwenye mechi ya kwanza iliyozikutanisha timu hizo jijini Paris, Ufaransa.

Chelsea ilihitaji kupigana toka nyuma mara baada ya kufungwa 3-1 kwenye mechi ya kwanza, Andre Schurrle ambaye aliingia mapema mara baada ya Eden Hazard kuumia alifanikiwa kuipa Chelsea bao la kuongoza ndani ya kipindi cha kwanza.

Huku zikiwa zimebaki dakika tatu mpira kumalizika Ba, ambaye pia aliingia, alifanikiwa kupiga mpira umbali wa mita sita na kuipa Chelsea goli la pili lililowapa nafasi ya kutinga moja kwa moja kwenye nusu fainali ya michuano hii.




No comments:

Post a Comment