Tuesday, March 11, 2014

Jack Bauer Arudi Upya na 24: Live Another Day - Sasa Kuwa na Episode 12 [Cheki Picha na Video]


KWA UFUPI:

Safari hii mashabiki wajiandae kuwaona
Jack na Chloe wakiwa paka na mbwa

Aliyekuwa ajenti wa Serikali Jack Bauer anaweza kuwa mtu asiyetambuliki nchini kwake Marekani, ila jambo la kushukuru ni kwamba, jamaa bado yupo mstari wa mbele katika kuisaidia Dunia akiwa jijini London. Hiyo ndivyo tamthilia mpya ya 24: Live Another Day itakavyokuwa kwenye awamu mpya inayotegemea kuanza kuonyeshwa mnamo May 5.

Sehemu ya series hiyo yenye episode 12 ambayo hutolewa na Fox inamtambulishakwa mara nyingine tena nyota wake maarufu Kiefer Sutherland ama Jack Bauer kwenye mapambano yake dhidi ya magaidi na waasi.

Ukweli ni kwamba kwenye series hii Jack Baur anakuwa ni ajenti asiyetambulika na Serikali ila anajaribu kuokoa mauwaji ya Rais yaliyopangwa kufanyika kwenye ardhi ya nchi nyingine.

Kwenye kipande cha series hii Benjamin Bratt ndiye anayeigiza kama mkuu wa CIA.








Icheki trela yake hapo chini...

No comments:

Post a Comment