Tuesday, May 28, 2013

Madawa Kupitiliza Yamuuwa Albert Mangwear, Afariki Afrika Kusini (RIPOTI KAMILI)

Albert Mangwear a.k.a Ngwear
Taarifa nilizozipata jioni hii zinasema kwamba mmoja kati ya wasanii wa siku nyingi wa Muziki wa kizazi Kipya Albert Mangwear a.k.a Ngwear amefariki Dunia akiwa nchini Afrika Kusini.
 
Chanzo cha kifo chake inaelezwa kuwa ni kutumia madawa ya kulevya kupitiliza.

Kwa kipindi sasa Msanii huyo alikuwa nchini Afrika ya Kusini, huku ikielezwa alikwenda huko kwa ajili ya kufanya show, mara baada ya kumaliza ziara yake aliamua kujikita kwa muda katika kile kinachosemekana kufanya michongo ya hapa na pale.

Taarifa zilizotumwa na mtu wa karibu aliyejiita Hussein Original ambaye yupo jijini Pretoria amesema kwamba Magwear amefariki leo asubuhi, Hussein amesema waliamka asubuhi na kuamua kwenda kuwaamsha wenzao na ndipo walipomkuta Ngwear akiwa amefariki huku M To The P akiwa hajitambui.

Hussein alisema "Mangwear alikutwa chumbani (Ghetto) akiwa tayari amefariki huku msanii mwenzake aitwaye M To The P alikutwa akiwa mahututi na hajitambui".

Aliongeza kwa kusema "mpaka sasa M To The P bado yupo hospitali na daktari amethibitisha juu kifo cha Ngwear".

Taarifa zaidi zimeeleza kwamba wasanii hao walikuwa wanategemea kurudi nyumbani Tanzania leo hii.
Ngwear Akiwa na M 2 The P
Mbali na mambo mengi Ngwear atakumbukwa kwa umahiri wake wa kuwa mkali wa mitindo huru (Free Style) kitu ambacho mpaka mwenyezi Mungu anachukua uhai wake inaaminika kuwa yeye ni mmoja kati ya waasisi wa mtindo huo kwa hapa Bongo.

Wimbo wa mwisho kwa msanii huyo kutoka rasmi redioni ni Ustake Beef (Yupo Juu) ambao alimshirikisha TID, mbali na huo Ngwear alifahamika na kutamba na nyimbo kama Ghetto Langu, Mikasi, She Gotta Gwan na nyinginezo nyingi za kwake na ambazo alizoshirikiana na wasanii wenzake.

Taarifa zaidi nitajitahidi kukufikishia kadiri ntakavyokuwa nazipata....

Mungu Ailaze Roho ya Marehemu NGWEAR Mahali Pema Peponi....!

4 comments:

  1. DAN MBN KUNA TAARIFA JAMAA HAJAFA UPI NI UKWELI?

    ReplyDelete
  2. Pengo lake halitazibika, jamaa alikuwa mkali wa free style, mtaratibu anaongea na kila mtu. mungu amempenda zaidi.

    ReplyDelete
  3. mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.bwana ametoa bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.

    ReplyDelete
  4. Dan Chibo, binafsi nimesikitika sana coz nilikuwa napenda sana nyimbo zake jamani hasa wa she gotta gwan, its me asnath wa tsj if u remember.Mungu ailaze roho yake mahali pema Amen.

    ReplyDelete