Tuesday, March 11, 2014

Kutana na Mapacha Wanaoshea Boyfriend Mmoja na Waliamua Kufanya Upasuaji Ili Wafanane kwa Kila Kitu [PICHA & VIDEO]


Mapacha hawa wenye umri wa miaka 28 Anna na Lucy DeCinque, walizaliwa na kupishana kwa dakika moja huku wakiwa wanashea kila kitu kwenye maisha yao - kuanzia kazi, gari, akaunti ya Facebook na hata boyfriend.

Ikiwa kama haitoshi kuzaliwa mapacha, wawili hawa wakaamua na kufanya upasuaji kiurembo kwa ajili ya kuondoa tofauti ndogondogo zilizokuwa zikiwatofautisha. Wanafanana kwa kila kitu kuanzia lips, matiti na nyusi za kuweka ambavyo vyote hivyo viliwagharimu £130,000.

Anna na Lucy, ambao wanaishi na mama yao, pia wanashea boyfriend ambaye wanaamini ndiye mtu sahihi kwao kimahusiano.



Anna alisema:

'Tunatoka na mvulana mmoja kwa sasa. Kuna watu watatu kwenye mahusiano yetu ambao tunashea kwa pamoja.'

Lucy akaongeza: 'Sio kitu cha ajabu kwetu. Tuna boyfriend mmoja na wote watatu tunashea kitanda kimoja. Kwa wanaume, kwenye mioyo yao hutaka kuwa na mademu wawili.

'Tuna radha moja kwa kila kitu, hivyo hututokea kumpenda mwanaume mmoja pia. Huwa tunakuwa pamoja tunapofanya mapenzi, hivyo kama tunampenda mtu mmoja, na tuache iwe hivyo. Kila mtoko ni lazma uwe ni wa mara mbili. Mara zote ni mara mbili au kisifanyike kitu.

Lucy alisema: 

'Mama yetu mara kadhaa alijaribu kututenganisha. Ila, baba yetu, sio kwa sana. Aliweza tu kusema, "je wewe ni yupi?" ''Huwa tunafurahi, hasa tulipokuwa wadogo. Tuliweza hata kubadilishana maboyfriend, kama tukiwa tumekwazika.

'Kama, hata tukiwa kwenye simu, kama ikiwa sitaki kuongea na boyfriend wangu, Anna aliweza kupokea simu na kujifanya yeye ndiye mimi. huwa tuliweza kufanya michezo ya namna hiyo, na mtu wa upande wa pili kushindwa kugundua. Ila kwa sasa tumepunguza tabia hiyo.'





Ben Byrne, fundi umeme, ndiye boyfriend wa Anna na Lucy kwa sasa

Angalia video yao wakiwa wanahojiwa....

No comments:

Post a Comment