Aliyewahi kuwa kipa wa timu ya Arsenal Jens Lehmann anaamini Bayern Munich wasingekuwa tishio na kushinda mfululizo kwa kiasi hicho kama wangekuwa wanacheza kwenye Ligi Kuu ya Uingereza.
Bayern wamepoteza pointi nne tu huku wakifunga wastani wa magoli matatu kwa mchezo mmoja katika mechi zao 24 walizocheza bila kufungwa kwenye Bundesliga msimu huu chini ya Pep Guardiola huku wakiwa kwenye harakati za kulitetea kombe walilolitwaa msimu uliopita.
Wakiwa wanaelekea kucheza mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Arsenal, Lehmann amehoji ubora wa timu za Ujerumni huku akiiona ligi hiyo kuwa inaboa.
Alipoongea na The Guardian, Lehman 44 alisema: "Naweza kusema upinzani wanaoupata kwenye Bundesliga sio mkubwa.
"Wapinzani wao hawafahamu namna ya kucheza nao. Hawatafuti hata njia za kujaribu.
"Bayern wasingekaa bila kufungwa kwenye Ligi ya Uingereza. Ubora wa timu za Premier League kwa upande wa kiwango ni mkubwa, hata kama ligi hiyo haipo juu.
"Kuangalia mechi za Buyern kwa kiasi flani inaboa pia."
No comments:
Post a Comment