Friday, May 10, 2013

Snoop: Niliwauza Makahaba Kwa Waburudishaji Na Wanamichezo

Snoop Akijiachia Na Makahaba
Rapa huyo ambaye ameamua kufanya muziki wa rege, aliwakusanya wanawake 10 walioridhia kwenye kundi, akiwaweka kwenye nyumba kisha kwenye basi huku akizunguka nao kwenye ziara ya Playboy mnamo mwaka 2003.

Nyota huyo ambaye anajulikana zaidi na jina lake la zamani kama Snoop Dogg – amekiri aliiweka ndoa yake na mpenzi wake wa toka shule aitwaye Shante Taylor kwenye hatari kwa kutendo chake cha kuwa anajiachia na mademu.

Amelieleza jarida la Rolling Stone, “Niliweka kampuni pamoja. Nilikuwa na gari likinifuata mimi likiwa na makahaba 10 ndani yake.

“Niliweza kumfuta kazi kahaba, kumlala kahaba, nikampata mwengine. Ulikuwa ndio utaratibu wangu. Mji kwa mji, chumba baada ya chumba, mwanamichezo kwa mwanamichezo, mburudishaji kwa mburudishaji.

“Nikiwa kwenye mji ambapo timu ya Denver Broncos au (Denver) Nuggets wakicheza, huwa nilikuwa nikipata wachezaji kibao waliokuwa wanakuja na kujiachia, kuchukua na kuchagua, na chochote kimoja ukipendacho na kukichochagua huwa kinakuja na hesabu.

“Wachezaji kibao walinunua makahaba kutoka kwangu.” alisema Snoop.

 

No comments:

Post a Comment