Saturday, May 11, 2013

Bosi Wa Kampuni Aamuru Wafanyakazi Watambae Katikati Ya Mji (PICHA)

Je ulidhani bosi wako ni mtu mbaya sana? Inawezekana yeye ni mtu mzuri, hasa ukijaribu kumlinganisha na bosi wa kampuni moja ya vipodozi ya nchini China ndani ya Chongqing.

Bosi huyo aliwaamuru wafanyakazi wake watambae kwa mikono na miguu kwenye kituo cha matangazo katikati ya mji, mbele ya mamia ya watu waliokuwa wanaangalia.

Tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 2 May, nakuonyeshwa live kwa wenye akaunti za microblog wa nchini China.

Baadae, picha zilichukuliwa na wapita njia kuonyesha unyanyasaji huo kwa wafanyakazi wakiwa wanatambaa kwa miguu na mikono yao, huku vichwa vyao vikiwa vinaangalia chini.

Baadhi ya watu waliwataarifu polisi juu ya tukio hilo, ambao walikuja na kusimamisha zoezi hilo.

No comments:

Post a Comment