Friday, February 21, 2014

INASIKITISHA SANA: Mzazi Amfunga Kufuli Mdomoni Mtoto Wake wa Miaka 4 Kisha Kumpiga Mpaka Kufa [PICHA]

Mahakama moja ya Ebute, kwenye Jimbo la Lagos, Nigeria imeamuru Chris Elvis, 30, andelee kubaki mahabusu kutokana na tuhuma zinazomkabili za kumuuwa mtoto wake mwenye umri wa miaka minne, Godrich Elvis, kwa kumfunga mdomo na kufuli kumpiga mpaka kufariki.

Muendesha mashtaka hayo, Bi S.O Solebo, alisema Chris ataendelea kukaa gerezani na kuuweka pembeni ushauri wa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai.

Ilielezwa kwamba Chris alimuuwa mtoto wake wa kiume katika kitendo kinachoonekana cha kishetani  na kuwa yeye ndiye aliyehusika kupelekea kifo chake.

Imeelezwa mahakamani hapo kwamba jamaa huyo anayefanya kazi ya ulinzi, alimfungia Godrich chumbani, kisha akimfunga mdomo kwa kufuli na kumpiga mpaka kufariki, ikiwa pamoja na kutumia chuma chenye moto mkali kumchoma mtoto huyo nyumbani kwao mtaa wa Adetola Adelaja, Meiran, kwenye jimbo la Lagos.

Chanzo kimoja kilimueleza muandidhi wa habari hii kwamba mtuhumiwa alikuwa akifanya vitu vya ajabu katika hali ya kuwashawishi polisi waamini kuwa mtoto yule alifarik sababu alikuwa anaumwa.

No comments:

Post a Comment