Nyota wa dancehall toka nchini Jamaica amehukumiwa kifungo cha maisha jela, bila ya kupewa nafasi kukaa rufaa ya mpaka atakapotumikia kifungo hicho kwa miaka 35.
Katikati ya mwezi March, Vybz (aliyezaliwa kama Adidja Azim Palmer), alikutwa na hatia kutokana na kitendo cha kumuuwa promota Clive "Lizard" Williams mnamo mwezi August, 2011.
Jamaa huyo mwenye miaka 38 amekaa mahabusu kwa kipindi cha miaka mitatu akiwa anasubiria hukumu yake, na mara baada ya mahakama kukaa kwa siku 65 za shauri hilo, hatimaye kura 10-1 zilimtia hatiani Kartel sambamba na watu wengine watatu.
Muendesha mashtaka alisema ushahidi ulijitosheleza kwamba William alipigwa mpaka kufa kwenye nyumba ya Kartel.
No comments:
Post a Comment