Mtoto mchanga raia wa China ambaye aliokotwa kwenye bomba la maji taka mara baada ya kuzaliwa ameruhusiwa kutoka hosptali na kukabidhiwa chini ya uangalizi wa bibi yake.
Ilichukua muda wa saa mbili kwa mtoto huyo kuokolewa katika maeneo yenye mkusanyiko wa watu wengi katika vyoo vya eneo hilo la Zhejiang lilopo jimbo la Pujiang, tukio ambalo lilivuta hisia za watu wengi duniani ambao wamekuwa tayari kumsaidia mtoto huyo ambaye ameruhusiwa kutoka hospitali jioni ya jumatano.
Kwa mujibu wa ofisi ya serekali za mitaa wamesema kwamba wameona kuwa hii ilikuwa ni ajali na kwa sababu hiyo mama wa mtoto aliyeokotwa atakuwa hana hatia.
Walezi wa mtoto huyo ambao ni bibi na babu wameshamchukua mtoto wakati mama wa mtoto bado yupo hospitali akipatiwa matibabu.
Kwa mujibu wa mama ambaye alitoa taaarifa jumamosi alisema kuna mtoto amekwama katika choo katika eneo hilo ambalo ni makazi ya watu na wakati akifanya usafi alisikia sauti ya mtoto mchanga akilia.
No comments:
Post a Comment