Monday, May 20, 2013

Kiasi Cha Fedha Ambazo Vilabu Vya Ligi Kuu Ya Uingereza Kila Moja Imepata Baada Ya Ligi Kuisha (LISTI)

Je ulidhani kwamba mechi za siku ya Jumapili za Ligi Kuu ya Uingereza ziliisha bure? Hebu fikiria tena.....

Timu kwenye Ligi Kuu ya Uingereza huwa zinapata mamilioni ya paundi kwenye siku ya mwisho, huku wengine wakiwa wanapata na wengine kukosa kwa kile walichotegemea kukipata siku ya mwisho.

Pia kuna kiasi cha hela kinachotokana na mapata ya televisheni, na kila aliye juu hupata zaidi ya mwenzake, huku kila anayekuwa juu ya mwenzake hupata kiasi cha paundi 750,000 zaidi.

 
Msimu uliopita, nafasi ya kwanza ilipata paundi milioni 15.1, wakati yule anayeshika nafasi ya 20 alipata paundi 755,000.

Kiasi cha Pesa Inachopata Kila Timu Kutokana na Nafasi Iliyoshika kwa Mujibu wa Takwimu za Msimu wa 2011 - 2012

Nafasi       
 Timu                      
Mechi     
Alama     
Hela Inazopata
1st
Manchester United
38
89
£15,101,240
2nd
Manchester City
38
78
£14,246,178
3rd
Chelsea
38
75
£13,591,116
4th
Arsenal
38
73
£12,836,054
5th
Tottenham
38
72
£12,080,992
6th
Everton
38
63
£11,325,930
7th
Liverpool
38
61
£10,570,868
8th
West Brom
38
49
£9,815,806
9th
Swansea
38
46
£9,060,744
10th
West Ham
38
46
£8,305,682
11th
Norwich
38
44
£7,550,620
12th
Fulham
38
43
£6,795,558
13th
Stoke City
38
42
£6,040,496
14th
Southampton
38
41
£5,285,434
15th
Aston Villa
38
41
£4,530,372
16th
Newcastle
38
41
£3,775,310
17th
Sunderland
38
39
£3,020,248
18th
Wigan
38
36
£2,265,186
19th
Reading
38
28
£1,510,124
20th
QPR
38
25
£755,062
 
Kimsingi ni kwamba, kwa mfano kwa ushindi ambao timu ya Fulham iliupata kwenye mechi yake ya mwisho wa 3-0 dhidi ya Swansea, iliiwezesha timu hiyo kupanda kutoka nafasi ya 15 mpaka ya 12, kitu ambacho kiliwezesha timu hiyo kujiongezea kiasi cha paundi millioni 2.25 kwa mujibu wa takwimu za msimu uliopita.

Waliopoteza hela nyingi zaidi kwenye siku ya mwisho walikuwa ni watoto wa Alan Pardew timu ya Newcastle, ambao walipoteza kiasi cha paundi millioni 2.26 baada ya kufungwa na Arsenal, kitendo kilichowafanya washuke toka nafasi ya 13th mpaka ya 16th.
 
 
 
 



No comments:

Post a Comment