Msanii wa mahiri katika tasnia ya filamu bongo Emmanuel Myamba sasa yuko mbioni kutoa filamu mpya kwa jina la “God’s Kingdom”. Myamba ameigiza zaidi ya filamu 43, tangu alipoingia kwenye sanaa mwaka 2004.
Alianza kuonyesha kipaji chake kwenye filamu ya kwanza ya Johari na iliyompa umaarufu ni filamu ya “Dar to Lagos”, ambayo ilimpatia tuzo ya Tanzania Film Vinara Award mwaka 2008.
Kupitia sanaa amepata mafanikio mbalimbali ikiwa ni pamoja na kujiajiri na kuendesha maisha yake mwenyewe, ana kampuni ijulikanayo kama Bornagain Films Production, pamoja na kutoa filamu zake binafsi kama ile ya “Pastor Myamba Trial”, ya pili ni “Pastor Myamba Temptation” na ile ya Comedy ya “Sometimes Yes Sometimes No”, mbali na kampuni ameweza kusambaza kazi zake binafsi.
Matarajio yake ni kufungua kampuni itayoitwa Tanzania Film Training Center, ambayo itatoa mafunzo kwa wasanii wa filamu Tanzania ili waigize kwa kuzingatie maadili, akiwa anaamini kwamba kuigiza nusu uchi siyo sanaa na kuwaponda wanaofanya hivyo kwani wanapoteza maana ya sanaa ya maigizo, kwa sasa anatoa kozi fupi kwa wasanii hao nakuwataka wahudhurie wote.
Pia amewataka wasanii kuacha tabia ya kukuza majina yao kupitia magazeti bali wafanye kazi nzuri ili wafahamike, na kuwataka wajifunze kupitia yeye.
“Tatizo la wasanii wa bongo sio wabunifu, ili kukabiliana na soko la kimataifa wanapaswa kuachana na tabia ya kujiamini kupita kiasi pale wanapopata majina makubwa sababu inafanya sanaa yetu kuwa na mambo yaleyale” Alisema Myamba.
Myamba anamzimia muigizaji Denzel Washington wa Marekani, na amejipatia umaarufu mkubwa kwa kuigiza kama Mchungaji, kitu ambacho yeye anachukulia kama huduma kwa Mungu na kwamba anamuinua Mungu kupitia sanaa yake.
Mara nyingi hupendela kuvaa bukta na t-shirt na viatu vya wazi anapokuwa katika mambo yake na anapokuwa home kwake, kama ukitaka kumpa zawadi anapendelea rangi ya chocolate, nyeusi na nyeupe. Japo mara nyingi napenda kuvaa kulingana na wakati na mazingira niliopo.
Sipendi kununua nguo kwenye duka moja kwani nahisi sitakuwa naendana na wakati, kuna wakati naagiza nguo nje ya nchi japo sipendi kuonekana kisharobaro napenda nivae simple lakini ni ng’ae.
Kilichomsukuma kuingia kwenye sanaa ni rafiki yake Steven Kanumba ambaye kwa kiasi kikubwa alimtia nguvu kwani hapo kabla hakua na wazo la kuwa muigizaji wa filamu.
Kwake rushwa ya ngono ni sumu, na kuwataka wanaofanya ivyo kutambua wanarudisha nyuma sanaa ya bongo.
No comments:
Post a Comment