Monday, May 20, 2013

Ni Katika Umri Gani Mama Anatakiwa Kuacha Kuvaa Nguo Mbele Ya Watoto Wake Wa Kiume..?


Mimi ni mwanamke niliyeolewa na nina miaka 34 nikiwa na watoto watatu, mdogo kuliko wote ana umri wa mwaka mmoja na mkubwa ana umri wa miaka 10.

Huwa nabaki mtupu mbele ya watoto hao wa kiume, huku nikiwa navaa nguo mbele yao nikiwa mtupu.

Nahitaji kujua kwamba ni sahihi kwangu kuwa navaa mbele ya mtoto wangu mwenye umri wa miaka 10, mtoto wangu wa pili ana umri wa miaka 3.

Je ni katika umri gani natakiwa kuacha kuvaa  au kuwa mtupu mbele ya watoto zangu wa kiume kama mama...?

No comments:

Post a Comment