Wednesday, April 17, 2013

Hatimaye Mourinho akubali kurudi Chelsea

Jose Mourinho
Baada ya kungoja kwa muda kwa muda mrefu hatimaye yametimia, Jose Mourinho amekubali kurudi na kuwa meneja wa Chelsea kuanzia msimu ujao, hii ni kwa mujibu wa gazeti la Daily Star la nchini Uingereza.
Kwa sasa meneja huyo ambaye anaifundisha Real Madrid ameshaandaa listi ya wachezaji ambao wataweza kuirudisha The Blues kwenye kilele mafanikio kwenye Ligi Kuu ya Uingereza, huku washambuliaji kama Hulk na Radamel Falcao wakiwa ni moja kati wachezaji ambao anataka kuja nao.
Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali, Mourinho atarudi Stamford Bridge mwishoni mwa msimu huu kwa mshahara utakaozidi ule anaoupata kwa sasa wa paundi million 12 kwa mwaka akiwa na Madrid.
Mourihno mwenye umri wa miaka 50 anafahamu fika kwamba Chelsea inahitaji nguvu za ziada ili iweze kuleta ushindani na timu kama za Manchester United, Manchester City, Arsenal na Tottenham.

No comments:

Post a Comment