Mbunge wa Kigoma Mjini Mh. Peter Selukamba (CCM) leo mchana
kwenye Kikao cha Bunge, alishindwa kuzuia nafsi yake
na kujikuta akitumia lugha isiyo rasmi kwenye kikao cha Bunge linaloendelea mjini Dodoma.
Mara baada ya Naibu Spika Mh. Job Ndungai kumpa nafasi ya kuchangia juu ya hoja ya
sakata la Lwakatare na Ulimbomka, Mh. Selukamba alijikuta akisema “FUCK YOU”.
Hii ni mara baada ya kuzongwa na minong’ono ya baadhi ya
wabunge, minong’ono ambayo ilikuja mara baada ya baadhi ya Wabunge kuona kwamba alichokuwa
anakiongea Mh. Serukamba ni propaganda
na marudio ya kile kile ambacho wabunge wengine walichangia.
No comments:
Post a Comment