Friday, April 04, 2014

Najisikia Faraja kwa Jay Z Kunipa Shavu Ndani ya Wimbo Wake - Lupita Nyong'o

Mara baada ya Lupita Nyong'o kupata taarifa kwamba mume wa Beyonce, Jay Z amempa shavu kwenye mstari wa verse ya  wimbo wa Jay Electronica, 'We Made It', mwigizaji huyo wa kike alifurahi sana.

Mshindi huyo wa tuzo ya Oscar hapo jana kupitia ukurasa wake wa Twitter aliandika vile anavyojisikia heshima kwa kutajwa kwenye wimbo huo na kujisikia kuwa ni sehemu ya utamaduni.

Licha ya kwamba ndani ya wimbo huo Jay akonekana kum-diss rapa wa Canadia, Drake lakini Lupita amethamini shavu alilopewa na Mr Carter.

Hii hapa ni tweet yake...


No comments:

Post a Comment