Brendan Rodgers anaamini bado hayupo tayari kusherehekea ubingwa wa Liverpool kwa kuweka bendera ya ushindi wa Ligi Kuu ya Uingereza katikati ya Anfield.
Jamaa huyu ambaye aliwahi kupanda mlima Kilimanjaro ameonya kwamba bado kuna kazi kubwa ya kufanya ili Wekundu hao waweze kusherehekea ubngwa wa Ligi Kuu kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 24.
Huku baadhi ya watu wakiona kwamba Liverpool ina nafasi ya kuchukua ubingwa yeye anaamini bado kuna kazi ya ziada na kama ni kupanda mlima basi ndio kwanza wako kwenye base camp.
Rodgers, ambaye alisaidia kuchangisha zaidi ya £13,500 kwa ajili ya kituo cha Marie Curie Cancer Care pale alipopanda mlima mrefu kuliko yote barani Afrika miaka mitatu iliyopita, amesisitiza kuna kazi ya ziada anayohitajika kuifanya ili aweze kusema Liverpool inaweza kuchukua ubingwa.
Chanzo: Daily Mirror
No comments:
Post a Comment