Tukio hilo limetokea kwenye Mtaa wa Olumo, Iwaya Onike, Yaba, kwenye Jimbo la Lagos nchini Nigeria, huku ikielezwa kwamba wakati tukio hilo likitokea mama wa mtoto alikuwa amemuacha mwanaye kwenye mikono ya mtuhumiwa aliyefahamika kwa jina la Bola Faleye ili aende kuoga.
Akiwa bafuni baada ya muda kidogo alisikia sauti ya kilio cha mwanawe hivyo akaamua kutoka bafuni na kumkuta mwanae akiwa tayari ameshakatwa vidole vyake viwili.
Haikuelezwa sababu za msingi zilizopelekea Mchungaji huyo kumkata videlo mtoto huyo, ila mwanzoni alipohojiwa alikana kuhusika na kitendo hicho, japokuwa mwishoni alipokuja kukamatwa na kubanwa na polisi alikiri kuhusika kufanya tukio hilo huku akiomba msamaha aachiwe.
No comments:
Post a Comment