Usain Bolt amekataa kuzikana ndoto za kuichezea timu ya Taifa ya Jamaica kwa upande wa mpira wa miguu, mara baada ya kuposti picha ya mfano wa gazeti kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Kulingana na taarifa zilizopo, nyota huyo wa Jamaica, inasemekana kuwa yupo tayari kupokea ofa ya Kocha wa timu ya Taifa hilo Winfried Schafer kama atamuita kwenye mechi za awali kwa ajili ya kufuzu michuano ya Kombe la Dunia kwa mwaka 2018.
Bolt aliweka picha ya ukurasa wa wa gazeti na kuiweka kwenye Instagram akiambatanisha na ujumbe usemao: 'Jamaica tunaonekanaje? Hmmm.. Tunasema kwa Ulimwengu na chochote kinawezekana'
Jamaa huyo mwenye miaka 27, ambaye ni mshabiki mkubwa wa timu ya Manchester United, alishawahi kuzungumzia juu ya shauku yake ya kuja kucheza kwenye timu hiyo ya Mashetani Wekundu.
Bolt akiwa jukwaa na skafu ya Manchester kwenye mechi dhidi ya Arsenal uliochezwa Old Trafford
No comments:
Post a Comment