Tuesday, January 21, 2014

Muigizaji wa Tamthilia ya Isidingo Lesego Motsepe Afariki Akiwa na Miaka 39 Baada ya Kuishi na Virusi vya HIV/AIDS kwa Miaka 15

Muigizaji Lesego Motsepe aliyejulikana kwa jina la "Letti Matabane" kwenye tamthilia maarufu ya nchini Afrika Kusini ya Isidingo amefariki Dunia.
Balozi huyo wa AIDS amefariki siku ya Jumatatu January 20, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na familia marehemu alikutwa amekufa nyumbani kwake Randburg, Afrika Kusini na kaka yake, Moemise, asubuhi ya saa tano kamili na kuthibitishwa na madaktari mida ya saa saba mchana.

Muigizaji huyo ameishi akiwa na virusi vya HIV/AIDS toka mwaka 1998 na amefariki akiwa na umri wa mika 39.

Mungu aiweke Roho yake mahala pema Peponi, Amen.

No comments:

Post a Comment