Tuesday, January 21, 2014

'Mtoto Yule ni Mbaya' - Joan Rivers Amchana Mtoto wa Kim & Kanye Aitwaye North West

Naona utani wa Joan Rivers unazidi kwenda mbali, na hii ni kutokana na kitendo chake cha kusema kuwa mtoto wa Kim na Kanye West ni mbaya. 
Joan alieleza jinsi vile Kim alipoenda na mtoto huyo kwenye ofisi za E! television network, sehemu ambayo yeye huwa anaendesha kipindi cha Fashion Police.

Hivi karibuni alipokuwa akiongea na watu pande za Saban Theater, Los Angeles, Joan alisema, 'mtoto yule ni mbaya... sijawahi kumuona mtoto wa miezi sita akiwa vile.'

Naamini Kanye hatoupata utani huu maana mmhh....

Mnaonaje hiki alichokisema Joan juu ya North West, toa maoni yako hapo chini.

No comments:

Post a Comment