Wednesday, May 15, 2013

Snura Akana Kuwa Na Bifu Na Shilole


Snura
Msanii wa filamu ambaye kwa sasa ameamua pia kujiingiza kwenye Muziki wa Kizazi Kipya Snura, amekana kwamba ana bifu na msanii mwenzake aitwaye Shilole.
 
Akizungumza na mimi mchana huu Snura alisema, watu wnajaribu kutengeneza mazingira kwamba yeye ana bifu na msanii mwenzake, ila ukweli ni kwamba hakuna kitu kama hicho.
“Kitu ambacho naweza kukizungumza, kwanza kabisa mimi sina bifu na mtu, na sitarajii kuwa na bifu na mtu”. Alisema Snura.
Huku akiongeza” Kwa sababu kwanza kwa jinsi nilivyo mimi nikimuona mtu anahitaji bifu kwangu mimi naongeza upendo kwake, hicho cha kwanza”.
“Nikirudi kwa upande wa Shilole mi nafikiri watu wanaongea  maneno wakihisihi kutokana na kwamba Shilole ametoka kwenye muvi akaingi kwenye mziki na mimi nimetoka kwenye muvi nimeingia kwenye mziki, na ndio wasichana aambao tumetoka kwenye muvi ambao tunaufanya.kwa hiyo lazima watu wan je watake kutupambanisha, watake kutuzungumzia, watake kufanya hiyo ambavyo wanafanya”.

“Ila ukweli uliopo kwamba, mimi sina bifu na mtu na sina bifu na Shilole na Shilole naongea nae tu vizuri”. Alimaliza Snura.

No comments:

Post a Comment