Tuesday, June 10, 2014

Jennifer Lopez Kutoimba Kwenye Ufunguzi wa Kombe la Dunia

Mwanamuziki Jennifer Lopez hatoweza kuimba wimbo rasmi wa Kombe la Dunia kwenye sherehe za ufunguzi wa michuano hiyo nchini Brazil, Fifa imetangaza.

Maafisa wamesema kwamba muimbaji huyo hatokuwepo kwenye onyesho hilo mnamo siku ya Alhamisi kwa sababu kiufundi ambazo hazijawekwa wazi.

Lopez alitegemea kuimba sambamba na rappa Pitbull na mwanamuziki wa Brazil Claudia Leitte, ambao kwa pamoja wametengeneza wimbo wa We Are One (Ole Ola).

No comments:

Post a Comment