Friday, May 10, 2013

Jay Z Kumsaini Neymer Wa Brazil


Jay Z
Rappa na mfanyabiashara Jay-Z  ambaye pia ni wakala wa kampuni mpya ya michezo, ana mpango wa kumsaini mchezaji nyota ya Brazil aitwaye Neymar.
Jarida moja la Kijerumani limeripoti kwamba Jay-Z na kampuni yake ya michezo ya Roc Nation, wapo kwenye mipango ya kuwaingiza kwenye mikataba wachezaji kadhaa wa Kibrazil, huku Neymer akiwa ni mchezaji  namba moja, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 anatabiriwa na wengi kuwa mchezaji nyota  toka Amerika ya Kusini.
Neymer
Neymar, ambaye anategemea kujiunga na klabu kubwa ya Barcelona ya nchini Hispania, ataungana na Robinson Cano wa New York Yankees na Skylar Diggins wa WNBA kwenye kampuni hiyo ya uwakala inayoyokua kwa haraka.

No comments:

Post a Comment