Hakikisha unawakwepa aina hii ya wanawake ili usijiingize
kwenye matatizo. Nitakwambia ni kwa nini…..
Demu wako wa zamani
Ni vizuri kutorudia mahusiano ya zamani na zaidi kama kwenye
mahusiano yenu ya mwanzo mambo hayakuishia kwa uzuri. Sababu kuu ya msingi, kiukweli
ni kwamba hakika mwanzoni mlikuwa hamuendani na ndio sababu ya iliyopelekea
kuvunjika kwa mahusiano yenu, ndani ya hizo sababu kuna vitu vilivyopolekea
kutokea kwa hayo, ukichunguza na kuziangalia kwa makini utagundua ni za asili
na ambazo si rahisi kwa mmoja wenu kuzibadilisha sababu ni vitu au mambo ambayo
yatakuwa ni ya damuni.
Dada wa rafiki yako kipenzi
Epukana na kujiingiza kwenye mahusiano na dada wa rafiki
yako. Si tu kwamba utaweza kujiingiza kwenye uhasama na chuki kama mambo
hayatakwenda sawa, ila pia utaweza kujiweka kwenye mazingira ya kujikuta siku
moja unapigwa hata ngumi za uso sababu tu ulimuumiza dada yake. Pia, utaweza
kumkosa mtu ambaye ndie alikuwa ni kimbilio lako kwa mambo mbalimbali pale
ambapo itatokea wewe na dada yake mambo kutokwenda sawa, sababu hapo patakuwa
na mgongano wa kimaslahi kwa huyo rafiki yako.
Wanawake wenye mambo mengi
Kiukweli, kutoka na watu kama hawa kinaweza kuwa ni kitu cha
kufurahisha, ila mwisho wa siku itakuingiza kwenye matatizo. Mara zote kumbuka
ni vyema kuwa salama kuliko kujuta. Usijiingize kwenye majaribu ambayo utakuja
kuyajutia kwa maisha yako yote.
Wanawake wanaopenda hela kupitiliza (Wachunaji)
Kuwa mbali nao, labda
kama unataka salio lako limalizike pasipo wewe kujifahamu. Naamini hili kila
mmoja analifahamu na halihitaji darasa zaidi.
Demu wa zamani wa rafiki yako
Kama unathamini urafiki wako na mshikaji wako achana na habari
ya kutoka na aliyekuwa demu wake. Mambo yanaweza kubadilika na kuwa kama au
zaidi ya yaliyotokea kwa rafiki yako na ikaja kula kwako zaidi. Wakati mwengine
inaweza tengeneza chuki kati yako na rafiki yako, huku akiamini kwamba ulikuwa
unatoka au kumnyemelea demu wake toka zamani.
Wadau mademu wapo wengi sana, fanya kutafuta wengine nje ya hawa…..
ni ushauri tu.
kweli
ReplyDelete1.hi ya kumrudia mpnz wako wa zamani sio kweli kabisa.coz kuna watu wanarudi wakiwa wamnyooka na kujirekebisha tabia ya mtu sio ngozi useme asibadilike...huo ni mtazamo wangu pia na nina ushahidi nao......
ReplyDelete2. kuhushu kutoka na dada wa rafiki yako hiyo ya kuchezea kichapo sio kweli ampigea au wapigane n what if we ndio mtemi sasa? hahahahaha
sijapenda mada yako haina jipya.rudi mezani uelimishe siyo bla bla.
ReplyDeleteHaya yote ni mapepo ya ngono, msaada na neema ya Mungu iliyo ktk Bw. Yesu Kristo inahitajika ili kushinda, vinginevyo kwa uwezo wa kawaida wa kibinadamu ni ngumu kujinasua - mpendwa c. Dsm
ReplyDelete