Wednesday, May 15, 2013

Chelsea Na Arsenal Kcheza Mechi Ya Ziada Kumpata Mshindi Wa Tatu EPL

Chama cha Soka nchini Uingereza kimesema kutakuwa na mechi moja ya ziada ili kuweza kumpata mshindi wa tatu wa Ligi Kuu ya nchi hiyo, kama ikitokea timu za Arsenal na Chelsea kuwa na rekodi zinazofanana.

Kama Chelsea watatoka droo ya 0-0 kwenye mechi yao ya mwisho na Arsenal kushinda kwa magoli 2-1, basi timu hizo zitakuwa zinalingana sawa kwa pointi, tofauti ya magoli na idadi ya magoli ya kufunga.

Na kama ikitokea hivyo na timu hizo kukutana mshindi wa mechi hiyo, moja kwa moja atakuwa amejikatia tiketi ya kushiriki hatua ya makundi kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya  kwa msimu ujao.

No comments:

Post a Comment