Tuesday, May 14, 2013

Abdul Kiba: Video Ya Kidera Kutoka Mwanzoni Mwa Mwezi Wa Tano

Abdul Kiba na Ali Kiba
Akizungumza na mimi kupitia kipindi changu cha The Takeover kinachorusha ndani ya TBC fm kila siku za wiki, msanii wa muziki wa kizazi kipya Abdu Kiba alisema kwamba, inambidi asubiri mpaka atakapokuja kufanya uzinduzi wa wimbo huo mwanzoni mwa mwezi wa tano.

Akiongeza Abdul Kiba alisema, "Video ya Kidera ipo tayari na ni video nzuri kuliko video zangu zote nilizowahi kuzitengeneza, washabiki wangu nawaomba waendelee kuisubiri, na mara baada ya uzinduzi wa wimbo na video hiyo basi wataiona kwenye luninga zao kuanzia mwanzoni mwa mwezi ujao".

Kidera wimbo ambao amemshirikisha kaka yake aitwaye Ali Kiba ni moja kati ya nyimbo ambazo kwa sasa zinafanya vizuri hasa kwa upande wa radio.

No comments:

Post a Comment