Tuesday, May 14, 2013

Nimemsaliti Mpenzi Wangu Na Mme Wa Mtu - Nashindwa Kumuacha Na Naomba Ushauri (BARUA)


Hodi humu ndani....,
Naomba nifiche jina langu kwa sasabu.....


Nimekuwa mgeni wa mara kwa mara ndani ya ukurasa huu, mpaka imefikia hatua nikaamua niwe mdau rasmi kwenye ukurasa huu na blog yake pia!
Ok, ngoja nirudi kwenye somo langu moja kwa moja, ila kwa kuanza napenda kutoa maelezo yangu mafupi na vile ambavyo awali nilikuwa.
 
Binafsi nilikuwa najiamini kuwa mimi ni mwanamke mwenye nidhamu, kanuni na aina ya mwanamkea ambaye huelewa maadili yake na viwango, kama mwanamke ninaejielewa na kujiheshimu.
 
Yote hayo, sababu nilikuwa ni mwanamke wa kufanya maamuzi ya haraka pasipo msaada wa mtu yeyote, kwa wastani ni mwanamke makini.
 
Kamwe, nilikuwa sielewi na nilishangaa ni kwa nini au inakuwaje wasichana huwa wanatembea na waume za watu, wanaume ambao wameoa na wao kufikia kiasi cha kujisahau na kujiingiza kwenye mapenzi motomoto!
 
Si tu kwamba niliona hali hiyo ni ya kujidharaulisha bali pia niliwaona wanawake wengi kama ni wapumbavu, wasio na mbele wala nyuma, wenye upeo mdogo, wenye ubinafsi na ukatili!
Mimi ni moja kati ya watu wenye sifuri ya uvumilivu kwa watu wadanganyi wa mapenzi, sababu niliwaona kama ni watu wenye ubinafsi na wasio fahamu maana ya maumivu.
Hata hivyo, nina kila sababu ya kubadili mitazamo yangu kama matokeo ya matukio kadhaa ya hivi karibuni ambayo yametokea katika katika maisha yangu!


Nasikitika kusema kwamba, kwa muda sasa nimekuwa nikimsaliti mpenzi wangu na mwanaume aliyeoa, hakika nina mshtuko mkubwa ndani yangu, na kitu kibaya zaidi ni juu ya ujinga ulionijaa kwa kujikuta nnaingia kwenye dimbwi la mapenzi na mume huyu wa mtu.
 
Mpenzi wangu na mimi ni watu ambao tupo karibu kwa muda mwingi, kwa kipindi chote cha miaka minne nilijiamini kwamba hakuna mwanaume mwengine ambaye ningeweza kuvutiwa naye.
 
Nimejaribu mara kadhaa kutaka kuachana na huyo mme wa mtu, sababu nafahamu fika kwamba ni ngumu kwa mimi na yeye kuweza kuwa na maisha ya pamoja, ila kiukweli naona inakuwa ngumu.

Sababu ya ujumbe huu ni nini hasa:
1) Ni kuwafahamishi wale wote ambao hawajaingia kwenye dimbwi hili kwamba, mnatakiwa kuwa makini msije mkatumbukia msipotegemea. Usije kusema hapana na haiwezekani, na usijione kwamba una nidhamu sana ama ni msafi au mwenye misimamo kiasi kwamba huwezi kujikuta unaingia kwenye vishawishi kama hivi. Kwa ambao wananifahamu mimi hawatoweza kuniamini kama kweli nimezama kimapenzi kwa mume wa mtu (Binafsi siamini kwamba imetokea hivi kwangu)
2) Japo huwa mnaseama kwamba mapenzi hayashauriki ila ni vyema kama ikija kutokea, jaribu kufuata ushauri kutoka kwa watu ambao wameshapitia mikasa kama hii.
Mfano mdogo unaoweza kuwa kama ule wako binafsi, mfano ambao mwazoni ulikuwa na mahusiano au upo kwenye mahusiano na unajua fika kwamba unahitaji kujiondoa kwa mtu ambaye unaifahamu kama hana na mapenzi ya dhati na unaishindwa...., hapo ndipo unapoona umuhimu wa ushauri.
Kitu ambacho binafsi nimekuwa nikikianya kwa sasa ni kusali na kujitahidi kutoonana na huyo mume wa mtu.  (Japo sitaki kukataa kwamba hujikuta nikiwa namfikiria). Japo pia nimemueleza mpenzi wangu kwamba nahitaji kupumzika!
Tafadhali naomba tujadili hili kiutu uzima, nikiamini kwamba kuna watu wengi  wana tatizo kama hili ila wanashindwa kumshirikisha mtu yeyote sababu wanaogopa aibu na lawama watakazotupiwa kutokana na tabia au kitendo hicho.
Asanteni

1 comment: