Wednesday, April 24, 2013

Mike Tyson Amtetea Suarez Kwa Kumng’ata Ivanovic

Mike Tyson
Bingwa wa zamani wa ngumi za uzito wa juuDuniani Mike Tyson, amemtetea mchezaji wa Liverpool Luis Suarez kwa kitendo chake cha kumng’ata mchezaji wa Chelsea Branislav Ivanovic.

Suarez ametozwa faini na klabu yaya Liverpool na anategemea kupewa adhabu na chama soka cha Uingereza, adhabu inayoaminika kuwa itakuwa ni ya kufungiwa kucheza mechi kadhaa kutokana na kitendo hicho, tukio hilo lilitoke wakati timu hizo zilipokutana na kutoka sare ya 2-2 kwenye uwanja wa Anfield.
 Kitendo kama hicho pia kiliwa kufanywa na Tyson kwenye pambano lake alilokuwa akipigana na Evander Holyfield mnamo mwaka 1997. Kupitia kipindi cha Glenn David nchini Marekani Tyson alikuwa na uhakika Suarez atamalizana na suala hilo.
“Nilimuona huyu jamaa kwenye Twitter na nikafikiria juu ya hatma yake itakuwaje,”  Tyson alisema, kwa kuwa mmoja kati ya wachezaji wenye wafuasi kwenye mitandao ya kijamii.
Akiongea na mtangazaji huyo Tyson alisema “Unajua kwamba jamaa alimng’ata mtu, sote tunajua kwamba upumbavu hutokea popote, nadhani  unafahamu nini namaanisha? Nina hakika atakuwa ameomba msamaha kwa huyu jamaa. Niliomba msamaha kwa  Evander na kila mmoja anaendelea na maisha yake.”
Suarez tayari ameshasema kwamba Ivanovic amekubali msamaha wake kutokana na kitendo hicho, japo kuna mapendekezo kwamba hiyo inaweza kuwa sio ishu ya msingi kuepekana na adhabu itakayomkabili.

No comments:

Post a Comment