Wednesday, April 24, 2013

Diamond Amlaumu Producer Kwa Kuvujisha Wimbo Wake, Kumuenzi Bi Kidude Kwa Kuimba Wimbo

Diamond Platnumz
Msanii wa miondoko ya Bongo Fleva Diamond Platnum, amesema atamuenzi  Marehemu Bi Kidude kwa kuimba moja kati ya nyimbo zake, Diamond amesisitiza kuwa wimbo atakaouimba utakuwa ni hit singo ambayo hata na yeye akija kufa jamii itambue kwamba alifanya kitu kwa ajili ya Bi Kidude.

Msanii huyo alizungumza hayo alipokuwa akiongea na mimi kupitia kipindi cha The Takeover cha TBC fm ambapo alisema “ntaimba nyimbo yake moja, ndio maana unaniona nipo nafanya research, kwa sababu nyimbo yenyewe ntakayoimba pia nataka niimbe na ibaki, hata mimi nikifa watu wanikumbuke kupitia nyimbo hiyo na ipendwe na watu pia.”

Katika hatua nyingine msanii huyo amewalaumu ma-producer wa nyimbo yake ya Mapenzi Basi, hii imekuja baada ya nyimbo hiyo kuachiwa bila ridhaa yake. Diamond amesema biashara ya kufanya kazi kiushikaji huwa inaponza sana na dawa yake ni kuacha kufanya kazi kindugu.
“Nimejisikia vibaya kinoma yani, nimeona kama nahangaika kufanya kazi halafu mtu kazi yangu anaichukulia masihala tu, lakini hiyo inatokana na kufanya kazi kindugu na marafiki studio” aliongeza na kusema “kwa sababu nyimbo kama ya Kesho hakuwahi kuvuja ilitoka ontime, lakini hizi kazi za kindugu ndugu ndio hupelekea watu kuvujishiana nyimbo kijamaa, yani sio freshi” alimaliza Diamond.
Wakati huo huo kutokana na kuvuja kwa nyimbo hiyo ya Mapenzi Basi na kukubalika kwa wimbo wake wa Ukimuona ambao nao ulivuja mara baada ya simu yake kuibiwa, Diamond ameruhusu rasmi kwa nyimbo hizo kuchezwa redioni.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba, haitakuwa na maana kuzizuia nyimbo zisichezwe redioni wakati tayari  nyimbo hizo tayari watu wanazo kwenye simu zao.
Amesisitiza kwa kusema “kama watu wakizichagua na kutaka zichezwe basi ni ruhsa kufanya hivyo” alisema Diamond.

No comments:

Post a Comment