Tuesday, April 23, 2013

Kanye Anatumia Hela Kubwa Aweze Kumuona Kim

Kim na Kanye
Kanye West kwa sasa anafanya kila linalowezekana kuhakikisha anampa sapoti mpenzi wake Kim Kardashian kwa kipindi chote cha ujauzito japo kwa sasa yupo jijini Paris kwa shughuli zake.

Kanye amekuwa akisafiri kwenye miji kadhaa kwa miezi sasa kwa ajili matukio, kuimba na kurekodi album mpya, ila hayp hayamzuii kuwepo kila ambapo Kim atahitajika kwenda kumuona daktari.

Tumeelezwa kwamba Kanye huwa anafanya safari japo tatu kwa kutumia ndege binafsi kutoka Paris kwenda L.A safari ambazo huwa zinatumia hela nyingi.

Chanzo hicho pia kimesema kwamba, Kanye amefikia hatua ya kwenda kuonana na dokta kwa ajili ya kupanga ahadi  mapema, ili aweze kupanga mambo yake ili aweze kuwepo pale Kim atakapohitajika kwa daktari.

 Kwa mujibu wa chanzo, Kanye amemsafirisha Kim kwenda Paris kwa ndege binafsi ili aweze kuwa nae kwenye muda wa ziada kabla ya Kim hajajifungua mnamo mwezi wa saba.

No comments:

Post a Comment