Thursday, April 18, 2013

Hips zake Don’t lie, Ila Ex-Boyfriend Wake ana Habari Nyingine.

Shakira na Ex-Boyfriend Antonio de la Rua
Aliyekuwa Boyfriend wa mwanamziki wa hit single ya Hips Don’t Lie aitwae Shakira, amefungua kesi ya madai dhidi ya mrembo huyo ambae kwa sasa anatokana mkali wa mpira wa miguu anayekipiga kwenye klabu ya Barcelorna ya Hispania aitwae Geralrd Pique.

Jamaa amefungua kesi ambayo anahitaji kulipwa kiasi cha Dola za Kimarekani 250 Millioni, huku dai lake kuu ni juu ya yeye kuhusika kwa kiasi kikubwa kwenye mafanikio ya mkali huyo wa Waka Waka.
Antonio de la Rua ameanzisha tifu la kimataifa dhidi ya ex wake, akisema kwamba yeye ndie ambaye amefanikisha kukuza “nembo ya Shakira”, huku akisisitiza kuwa alihusika kwenye mafanikio ya ngoma zake mbili ambazo zimemuweka juu mdada huyo, akizitaja ngoma za Hips Don’t Lie” na “Waka Waka” kuwa kuna mkono na akili zake zilihusika katika kufanikisha mafanikio ya ngoma hizo.


No comments:

Post a Comment