Thursday, April 18, 2013

Bi Kidude Kuzikwa Leo

Marehemu Bi Kidude
MSANII mkongwe na gwiji wa muziki wa taarabu na ngoma za muziki asili ya pwana, Fatma binti Baraka Hamisi maarufu kama ‘Bi Kidude’, aliyefariki jana mchana majira ya saa saba nusu, anatarajia kuzikwa leo nyumbani kwao Unguja kwenye Makaburi ya Kitumba.
Bi Kidude alifariki jana Jumatano, huku chanzo cha kifo chake kikielezwa kuwa ni maradhi ya kiuskari yaliyopelekea kusababisha uvimbe kwenye Kogosho.
Bi Kidude Akionyesha Umahiri Wake wa Kupiga Tumba
Kwa mujibu wa mmoja kati ya wajukuu zake aitwae Omari alinieleza kwamba Bi Kidude amefariki siku ya Jumatano mnamo saa saba na nusu mchana.

Akiendelea kuongea Omari alisema "takribani miezi mitano iliyopita, marehemu alikuwa anasumbuliwa na kisukari, kilichomsababishia kupata uvimbe mwilini mwake."
Aliongeza kwa kusema, kwa kipindi chote hicho walijaribu kumpeleka hospitali ila hali yake haukutengemaa mpaka umauti wake ulipomkuta.
Bi Kidude Enzi za Uhai Wake Akiwa Anaimba
Bi Kidude amefariki dunia nyumbani kwa watoto wake Bububu, nje kidogo ya mji wa Unguja na anategemea kuzikwa leo nyumbani kwao Unguja kwenye Makaburi ya Kitumba.

No comments:

Post a Comment