Thursday, April 18, 2013

Jamaa amuoa Dada yake wa Damu baada kutembea nae kwa Miaka 12

Prosper Dzakpasu
Jamaa mmoja aitwae Prosper Dzakpasu wa kijiji cha Dzodze Ablorme kilichopo Ketu, Kusini mwa Volta nchini Ghana, ameripotiwa kuishi kinyumba na dada yake wa damu kwa miaka 12 sasa.

Licha ya tahadhali na vitisho vya watu mbalimbali, Prosper, 38, amegoma kuacha kulala pamoja na dada yake.

Vyanzo karibu na familia vilielezea gazeti la DAILY GUIDE kwamba, baada ya kugundua hali hiyo walimkanya, ila kutokana na kukaidi kwake ndipo ilipowapelekea kuijulisha jamii juu ya swala hili.
Waligundua juu ya huo mwenendo, hata Mama wa watoto hao naye alikuwa na shaka juu mwenendo wao, kwa mara kadhaa aliwataka  waachane na tabia hiyo. Ila licha ya jitihada zake Mama mzazi wa watoto hao alichoka na kuamua kukaa kimya.

Prosper ni mtoto wa kwanza miongoni mwa watoto watano kwenye familia, wakati Cynthia ni mtoto wa mwisho kuzaliwa.

Babu yake na Prosper, ambaye pia aligundua hali hiyo, mara kadhaa na kwa wakati wake alijaribu kuwakanya lakini ilishindikana.
Watoto wengine watatu nao hawakuwa wamependezwa na mwenendo huo na hawakuwa na namna yoyote kuweza kuzuia mahusiano hayo yasiendelee.
Inasemekena Prosper alianza kutembea na dada yake, Cynthia Dzakpasu, ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 29 kipindi ambacho alikuwa na miaka 17.
 Mahusiano hayo ambayo yalianza taratibu, yalikuwa sio siri, kwani kipindi hicho walikuwa wanaishi kama mke na mume, wakiwa wanaishi pamoja sehemu moja iitwayo Dzodze Ablorme, huku Prosper akiwa anjishughulisha na kazi za kushona nguo.
Baada ya kuonywa mara kadhaa na watu kwenye familia yao ambao mwanzoni walikuwa wanaificha hali hiyo, Prosper peke yake akaamua kupotea pasipojulikana kwa miaka mitano.
Baadae ikaja julikana kwamba alikimbilia Accra kwenda kufanya kazi, baada ya wiki chache, alikuja kumchukua dada yake na kwenda kuishi kwenye nyumba ambayo haikufahamika jijini Accra.
Hakuna ambacho kilifahamika mpaka mwaka mmoja uliopita walipoamua kurudi Dzodze wakiwa na mtoto wa kike mweye miaka sita.
Chanzo hicho kiliieleza DAILY GUIDE kwamba “Prosper kwa sasa amezidi kuwa kiburi na anaonekana kutomuheshimu au kumuogopa tena mtu yoyote. Kwa maana anajua mtu yeyote atakapo kutana nae au kumuita itakuwa anataka kuongea juu ya uchafu wake, kwa hiyo hatokuja na hata akija hatomjali mtu yoyote kwa lolote atakalolisema.”
 Chanzo hicho kimeeleza, familia imeamua kulifikisha suala hilo Polisi ili Prosper akamatwe na kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa wa sheria za nchi.
Baadhi ya ndugu, ambao walishindwa kuelewa kwanini ndugu hawa wameamua kujiingiza kwenye mahusiano haya ya ajabu, wamehusisha kitendo hiki ni masuala ya nguvu za giza, wakati wengine wamehusisha kitendo hicho na laana.

No comments:

Post a Comment