Picha iliyopigwa na mpiga picha wa Sportsmail, Kevin Quigley, imeshinda tuzo ya picha bora ya Premier League kwa msimu uliopita, pale alipompiga nahodha wa Liverpool Steven Gerrard alipokuwa akishangilia mara baada ya kufunga kwenye mechi ya ugenini walipocheza na Fulham msimu uliopita.
Wapiga picha wote mahili walikaribishwa kutuma picha zao bora za kipindi chote cha ligi, picha ambazo zilihakikiwa na jopo la wataalamu, ambapo ndani yake miongoni mwa waliotuma picha zao akiwemo wapiga picha mahiri kama Martin Tyler, Dave Shopland, Andy Dunn na Alan Sparrow.
Quigley alishinda miongoni mwa wote waliotuma kwa picha hii aliyoipiga wakati nahodha wa Liverpool akiwa anashangilia kwenye uwanja wa Craven Cottage ikiwa ni dakika za lala salama katika mechi iliyoisha kwa Liverpool kupata ushindi wa 3-2 mnamo mwezi February.
No comments:
Post a Comment