Saturday, December 21, 2013

Waoana Hadharani Wakiwa Uchi wa Mnyama Huku Umati wa Watu Ukishuhudia [PICHA]


Wanandoa wawili walikamtwa kwenye siku ya harusi yao baada ya kufunga ndoa wakiwa uchi wa mnyama mtaani katika kile kilichosemekana ni kampeni yao kupinga sheria ya San Francisco inayokataza watu kuwa watupu.

Bibi harusi Gypsy Taub, 44, na bwana harusi Jamyz Smith, 20 walikamatwa ndani ya dakika chache baada ya kubadilishana viapo.

Kwa mujibu wa Taub:  'Hii ni katika kupinga sheria ya utupu, najua watu wa wapo nyuma yangu.'

Harusi hiyo iliendeshwa na mwanaharakati anayetetea kufutwa kwa sheria ya utupu aitwaye George Davis, wa Kanisa la Universal Life.

Mara baada ya kusoma kutoka kwenye kitabu chake Kitakatifu, kinachoitwa 'Erotic Art,' Davis alisema: 'Natangaza kuwa ninyi ni mke na mume.'

'Watu husherehekea kwa njia yoyote wanayojisikia kuwa poa nayo, mmoja kati ya watu waliowatakia mema wanandoa hao alisema, akiongeza: 'Ni kitu kizuri wanachokifanya. Hakuna aliyeumizwa. Hakuna aliyeathiriwa.'

Angalia picha hapo chini....






No comments:

Post a Comment