Friday, February 07, 2014

TENDO LA NDOA; Tiba Mbadala ya Maradhi ya Moyo, Ubongo, Maumivu ya Kichwa?

“Kwa mfano, tendo la ndoa linaondoa msongo wa mawazo iwapo unayetenda naye unampenda na  amekupa maandalizi mazuri. Sidhani kama alimradi utende hilo tendo na yeyote litakusaidia,” anasema mtaalamu huyo. 
KWA UFUPI:

    Ikumbukwe kuwa utafiti
hauchochei watu kufanya
mapenzi kiholela, bali unajikita 
kwa  wanandoa pekee.

Ingawa tendo la ndoa lisipofanywa kwa kuzingatia kanuni na taratibu, sambamba na umakini, linaweza kusababisha maradhi, lakini kwa wanandoa, tendo  hilo linatajwa kuwa na manufaa mengi  kiafya tofauti na faraja ya kawaida iliyozoeleka kwa wengi.
Imefahamika kuwa tendo hili likifanyika ipasavyo husaidia kuondoa msongo wa mawazo, maradhi ya moyo, maumivu ya kichwa yasiyokoma na kupunguza kasi ya saratani ya tezi dume.

Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba Muhimbili (Muhas), Dk Yahya Kishashu anasema inategemea tendo linafanywa na nani na mhusika yupo kwenye mazingira gani.

“Kwa mfano, tendo la ndoa linaondoa msongo wa mawazo iwapo unayetenda naye unampenda na  amekupa maandalizi mazuri. Sidhani kama alimradi utende hilo tendo na yeyote litakusaidia,” anasema mtaalamu huyo.

Anaongeza kuwa  ndiyo maana baadhi ya watu wanatoka nje ya ndoa zao kwa sababu si mara zote tendo la ndoa linawafurahisha wanandoa.

“Wakati mwingine tendo hilo laweza kuwa karaha kwao,” anasema

Mazoezi

Si hivyo tu, utafiti uliofanyika Canada  hivi karibuni umebainisha kuwa kufanya tendo la ndoa kwa kipindi cha dakika 25 kwa wanamume kunachoma kalori 100 na kwa wanawake kalori 69.

Tendo hilo likifanyika kwa nusu saa, linaweza kupunguza kalori za mwili kuliko kutembea kwenye mashine ya mazoezi ya ‘treadmill’.

“Ni sawa na kucheza mpira wa tenisi au kutembea ukipanda mlima kwa dakika 20 au kucheza gofu kwa kasi kwa dakika 33 au zoezi la yoga kwa dakika 40,” sehemu ya utafiti hiyo inasema.

 Utafiti huo wa Canada ulishabihiana na kampeni  iliyofanywa na Taasisi ya Moyo ya Uingereza ambayo ilisema kuwa  dakika 30 za tendo la ndoa kwa siku ni muhimu kama mazoezi ya kutembea kwa mashine.

Kwa undani zaidi utafiti huo ulichambua na kusema kuwa, tendo la ndoa, lina manufaa  kwa moyo na mapafu.


Inaelezwa kuwa vichocheo  vinavyotoka  baada ya tendo la ndoa vinasaidia kupunguza kiwango cha msongo wa mawazo na kuongeza  uzalishaji wa seli mpya za ubongo.

 Kuhusu mazoezi, Dk Kishashu anasema anakubaliana na utafiti huo na kusema kuwa ni kweli tendo hilo linasaidia kupunguza kalori, lakini linapofanyika mara nyingi zaidi linazeesha.


Hata hivyo, wanasayansi wanalipa uzito mdogo tendo hilo katika muktadha wa ujenzi wa hisia na mwili na kuwa halisisitizwi vya kutosha kama aina mojawapo ya mazoezi.

CHANZO: Gazeti MWANANCHI 

Habari kamili fuata link hii >>>> http://www.mwananchi.co.tz/Tendo-la-ndoa--Tiba-mbadala-ya-maradhi-ya-moyo--ubongo-/-/1596774/2196600/-/3p5i0c/-/index.html

No comments:

Post a Comment