Wednesday, January 22, 2014

Akiwa na Miaka 30 tu Mido Achaguliwa Kuwa Kocha Mkuu wa Zamalek ya Misri

Mchezaji wa zamani wa Tottenham Hotspur na mshambuliaji wa Misri Ahmed 'Mido' Hossam ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa klabu ya Zamalek.

Mido mwenye umri wa miaka 30 ndiye kocha mdogo kuwahi kutokea katika historia ya soka la Misri huku akichukua nafasi ya Helmi Toulan.

Mido, alianza kucheza mpira akiwa na Zamalek, amepinga wanaobeza kwamba yeye ni mdogo sana kuwa kocha

"Kwa wale wanaobeza kuchaguliwa sababu ya umri wangu, ni kitu cha kawaida ukiwa Ulaya na nipo tayari kwa ushindani," alisema kupitia TV ya Misri.

"Hasa kama nilivyokuwa kiongozi uwanjani kama mchezaji.

"Nilikataa kufundisha timu ya vijana ya Paris Saint-Germain, timu ya Masry ya Misri na ofa nyingine ambazo nilizikataa yote ili niweze kuja kuifundisha timu ninayoipenda kwa dhati."

Chanzo: BBC Sports

No comments:

Post a Comment