Sunday, December 08, 2013

Makamu wa Rais Nchini Sudan Ajiuzuru - Bashir


Rais wa Sudan Omar al-Bashir ametangaza kujiuzuru kwa makamu wa Rais wa nchi hiyo Ali Taha mnamo siku ya Jumamosi.


Taha alikuwa anashika nafasi hiyo ambayo kisiasa ni ya pili kiukubwa kwa nchi hiyo na ndiye aliyekuwa muhimili wa nchi hiyo katika mapatano juu ya makubaliano ya amani ya Sudan ya mwaka 2005 ambayo yalipelekea kuisha kwa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

“Amejiuzuru ili kuacha nafasi kwa vijana na hakuna matatizo kati yetu,” taarifa ya Ikulu ilimnukuu Bashir akisema.

No comments:

Post a Comment