Saturday, December 07, 2013
Kombe la Dunia Brazil Mechi Kuwa na Mapumziko Ndani ya Mchezo (Timeouts)
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) Jerôme Valcke, amesema kama ikitokea kwenye mechi wakati inaendelea na kukawa na joto kali, michezo kwenye baadhi ya mechi za Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil inaweza kusimamishwa mara moja au zaidi ili kuwaruhusu wachezaji wapumzike kutokana na joto.
"Kila mechi itakuwa na mratibu, daktari na refa wa mchezo. Watu hawa watatu watachukua hatua za msingi kuhakikisha mazingira yanayokubalika na watakuwa na amri ya kusimamisha mechi kwa ajili mapumziko", alisema Valcke, ambaye siku mbili zilizopita amekiri pia kwamba michuano hiyo ya Brazil 2014 itakuwa ni ya Kombe la Dunia lenye joto kali.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment