Friday, December 20, 2013

Luis Suarez Asaini Mkataba Mpya na Liverpool


Mshambuliaji wa timu ya Liverpool Luis Suarez amesaini mkataba mpya wa muda mrefu na klabu hiyo.

Suarez, ambaye alijiunga na Reds mwezi  January 2011, ameshafunga magoli 17 katika mechi 11 alizocheza kwenyePremier League.

Suarez, ambaye kwenye mkataba wake ambao ulikuwa uishe mwaka 2016, atakuwa akilipwa kiasi cha £160,000 mpaka mwisho wa msimu na baada ya hapo atakuwa akipokea kiasi cha £200,000 kwa wiki mpaka mwisho wa mkataba wake wa miaka minne.

"Ni furaha yangu kukubali kuingia mkataba mpya na Liverpool na maisha yangu ya mbele yatakuwa salama kwa kipindi kirefu. Tuna wachezaji wazuri na timu inazidi kukua kila wakati," alisema mchezaji huyo mwenye miaka 26 sasa.

"Naamini nitafanikiwa malengo yangu ya kushinda mataji na kucheza kwenye kiwango cha juu na Livepool. Lengo langu ni kuisaidia kuweza kufika pale haraka itakavyo wezekana."

Chini picha Sarez aliposaini mkataba wake...






No comments:

Post a Comment