"Uamuzi wakustaafu ni suala ambalo nilifikiria na kuliona ni kitu kikubwa sana. Ila ni muda muafaka". Ferguson alisema.
Wacheza kamari wengi wamekuwa wakimuhusisha na kumpa nafasi kubwa Jose Mourinho, ambaye amekuwa mtu mwenye nafasi kubwa kuchukua nafasi hiyo, ila kupitia vyombo mbalimbali vya habari likiwemo gazeti la Sportsmail, taariza zinaeleza kwamba kocha wa Everton David Moyes anaweza kuwa mrithi wa kiti hicho.
Mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 71 anajiandaa kuuaga umati wa mashabiki timu hiyo Uwanja wa Old Trafford Jumapili mara baada ya mechi ya United dhidi ya Swansea.
Anategemea kufanya hivyo kwenye mechi ambayo timu hiyo itakabidhiwa taji la ubingwa wa Ligi Kuu England kwa msimu huu, hilo likiwa ni taji la 13 chini ya Ferguson.
Mazungumzo yanaendelea katika kumsaka mrithi wake huku kocha wa klabu ya Everton, ambaye ni Mskotishi mwenzake David Moyes kuwa ni chaguo la kocha huyo kama ndiye mrithi wake.
Ferguson amewashukuru watu mbalimbalia ambao walimsaidia kuweza kuijenga timu kutoka kwenye timu ambayo hakuwahi kuchukua taji kwa zaidi ya miaka 26, mpaka kuwa moja kati ya timu kubwa sana duniani.
"Ni lazma nitoe shukrani zangu kwa familia yangu kwa upendo na ushiriki wao umekuwa kitu muhimu," aliongeza Fergie.
"Mke wangu Cathy amekuwa ni mtu muhimu sana katika maisha yangu na kazi zangu za soka, pia na kwa wachezaji pamoja na wafanyakazi wengine, wale wa zamani mpaka sasa, napenda kuwashukuru wote kwa uwezo wa juu wa kitaaluma walioutoa katika kufanikisha yote yaliyosaidia kutwaa makombe mbalimbali. Bila mchango wao historia ya klabu hiiisingekuwa kubwa kiasi hiki".
Mataji Aliyoshinda Alex Ferguson Akiwa Na Man Utd
Premier League: 1993, 1994, 1996, 1997, 1999, 2000, 2001, 2003, 2007, 2008, 2009, 2011, 2013.FA Cup: 1990, 1994, 1996, 1999, 2004
League Cup: 1992, 2006, 2009, 2010
Champions League: 1999, 2008
Cup Winners Cup: 1991
Fifa Club World Cup: 2008
Uefa Super Cup: 1992
Inter-Continental Cup: 1999
FA Charity/Community Shield: 1990 (shared), 1993, 1994, 1996, 1997, 2003, 2007, 2008, 2010, 2011
Swali la msingi, JE MANCHESTER UNITED ITAWEZA KUWA MANCHESTER BILA SIR ALEX FERGUSON...?
No comments:
Post a Comment