Wednesday, May 08, 2013

Adhabu Wanazopewa Wanawake Wanapofamaniwa Kwa Nini Haiwi Hivyo Kwa Wanaume?

Mwanamke mmoja aliyekuwa ameolewa, amejikuta akipigwa na kudhalilishwa kwa kuvuliwa nguo kwenye sehemu ya wazi mara baada ya kufumaniwa akiwa na mwanaume mwengine.

Swali langu ni kwamba, ni kwa nini wanaume huwa hawapewi adhabu kama ambazo wanawake wengi hupewa pale wanapokuwa wamefumaniwa na mwanaume mwengine?

Hukumu hutolewa mara moja pale ambapo mwanamke akifumaniwa, bila ya watu kuuliza sababu zilizompelekea kufanya hivyo, moja kwa moja huonekana na kuuhukumiwa kama ni malaya, na kupewa kila aina ya majina ya kumdhalilisha. Na pia wakati mwengine kupewa kupewa adhabu kama hii tunayoiona, kupigwa kuvuliwa nguo na kudhalilishwa kwenye jamii.

Swali lingine, ni kwa haki gani aliyonayo binadamu wa kawaida aweze kumuhukumu binadamu mwenzake kwa yale aliyoyatenda au kuyakosa?


Watu wengi ni wepesi wa kutoa hukumu kwa wengine, huku wakijua fika kwamba wao wenyewe kama walishawahi kufanya kitu kama hicho au watakuja kufanya aina hiyo hiyo ya kosa na huenda ikawa ni zaidi ya alivyofanya huyo ambaye wamemuhukumu.

Watu wana tabia ya kuzitanguliza Dini zao huku wakifahamu fika kwamba hizo Dini zao zinakataza binadamu kuhukumu binadamu mwenzake. Je hukumu sio kwamba hutolewa na Mungu pekee?

Tafadhali, kuwa huru kushirikisha mawazo na upeo wako juu ya hili.

No comments:

Post a Comment